IQNA

Saudia yaorodheshwa kama muuaji watoto baada ya kuwaua watoto Yemen

10:27 - October 07, 2017
Habari ID: 3471207
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa hatimaye umeiweka Saudi Arabia katika orodha nyeusi ya nchi zinazokiuka haki za watoto duniani kutokana na mauaji yanayotekelezwa na Jeshi la Saudia na waitifake wake dhidi ya watoto wa Yemen
Ripoti hiyo iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Alkhamisi inasema muungano unaoongozwa na Saudia umehusika na mauaji ya watoto nchini Yemen.
Ripoti hiyo imesema Saudia na waitifaki wake waliuawa watoto 683 nchini Yemen mwaka 2016 mbali na kushambulia shule 38 nchini humo.
Waitifaki wa Saudia katika jinai hizo dhidi ya watoto wa Yemen ni pamoja na Bahrain, Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri, Jordan, Morocco, na Sudan.
Akizungumzia suala hilo hapo siku ya Alkhamisi, Muhammad Abdu Salaam, msemaji wa harakati ya wananchi ya Ansarullah ya nchini Yemen amekosoa vikali upendeleo na uzembe ambao umekuwa ukifanywa na Umoja wa Mataifa katika kuiweka Saudia katika orodha ya nchi zinazokiuka haki za watoto duniani na kusisitiza kwamba kwa uzembe wake huo, Umoja wa Mataifa inaishajiisha nchi hiyo iendelee kukiuka haki za watoto wa Yemen. Vita vya kichokozi vya Saudi Arabia vilianza mwezi Machi 2015 na sasa vimeingia katika mwezi wake wa 30, ambapo watotoa wasiokuwa na hatia ndio wahanga wakubwa wa vita hivyo.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwishoni mwa mwezi Julai na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa Unicef, Wayemen milioni 20 na laki saba wanahitajia misaada ya dharura ya kibinadamu kutokana na vita hivyo ambapo milioni 11 na laki tatu kati yao ni watoto. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto karibu 1700 wameuawa na wengine karibu 2800 kujeruhiwa katika vita hivyo. Watoto wengine karibu milioni 2 wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo. Watoto karibu milioni 2 hawaendi shuleni na wengine karibu milioni moja wamefanywa kuwa wakimbizi katika maeneo tofauti ya Yemen.

Katika orodha ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa kuhusu wakiukaji wa haki za watoto dunaini, ni muungano tu wa kijeshi unaoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen  ndio umetajwa moja kwa moja kuhusika na ukiukaji wa haki za watoto wa Yemen na wala sio Saudia kama ilivyokuwa katika orodha ya mwaka jana. Kwa maelezo mengine ni kuwa Umoja wa Mataifa kwa upande mmoja unakiri kwamba Saudia inahusika moja kwa moja katika ukiukaji wa haki za watoto wa Yemen na kwa upande wa pili kukwepa kutia jina la nchi hiyo katika orodha ya nchi zinazokiuka haki hizo.
3464091

captcha