IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu katika chama tawala nchini Uingereza

1:12 - August 10, 2018
Habari ID: 3471622
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekosolewa upya kwa kutochukua hatua za kutosha za kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia katika chama chake cha Wahafidhina (Conservative).

Kufuatia ukosoaji huo May amelazimika kumtaka waziri wake wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson aombe msamaha kwa kuwavunjia heshima wanawake Waislamu wanaovaa Burqa au Niqab.

Johnson hivi karibuni alisema wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu wanashabihiana na 'wezi wa benki' na 'masanduku ya barua'.

Taasisi ya Tell MAMA ambayo inaweka orodha ya vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu Uingereza imesema Chama cha Wahafidhina hakijachukua hatua yoyote ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu miongoni mwa wafuasi wake.

Mwanzilishi wa Fiyaz Mughal amebainisha masikitiko yake kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza hakuchukua hatua za kukosoa matamshi ya Johnson. Aidha, Mughal amelaani vikali matamshi ya Johnson na kusema yamekuja wakati ambao Waislamu tayari wanakabiliana na hali mbaya zaidi ya hujuma dhidi yao katika miaka ya hivi karibuni.

Mwezi Junia zaidi ya misikiti 350 na jumuiya za Kiislamu nchini Uingereza zimetaka uchunguzi ufanyike kuhusu chuki dhidi ya Uislamu miongoni mwa wanachama wa ngazi za juu wa chama tawala cha Conservative.

Baraza Kuu la Waislamu Uingereza,MCB, hivi karibuni liliandikia barua chama cha Conservative likitaka uchunguzi kamili ufanyika kuhusu vitendo cha chuki dhidi ya Uislamu katika chama hicho.

Kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya watu Uingereza, kuna Waislamu milioni 2.8 kati ya watu milioni 64 nchini humo.

Pamoja na mchango wao mkubwa na wa kihistoria, Waislamu Uingereza wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa za kubaguliwa na kutengwa na watu wenye misimamo mikali ya utaifa na chuki dhidi ya Uislamu.

3466505

captcha