IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hakutatokea vita na hatutafanya mazungumzo na Marekani

22:13 - August 13, 2018
Habari ID: 3471628
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matamashi na lugha zisizo na adabu za viongozi wa Marekani kuhusiana na vikwazo, vita na mazungumzo na Iran kusema kuwa, tunasisitiza kwamba, hakutatokea vita na hatutafanya mazungumzo.

Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo asubuhi ya leo alipoonana na maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali ambapo amesisitiza katika hotuba muhimu aliyoitoa kwamba, hakutatokea vita kwani sisi kama ilivyokuwa huko nyuma hakuna wakati ambapo tulianzisha vita na Wamarekani hawatothubutu kuanzisha vita kwani wanafahamu vyema kuwa, vita hivyo vitakuwa ni kwa madhara yao, hasa kwa kutilia maanani kwamba, Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran limethibitisha kwamba, litatoa pigo kubwa mno kwa kila mvamizi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia suala la mazungumzo na Marekani na kusisitiza kwamba, taifa la Iran halitofanya mazungumzo na Wamarekani hasa kutokana na kuweko ushahidi wa wazi, tajiriba ya huko nyuma na madhara makubwa ya kufanya mazungumzo na dola ghushi na lenye kutumia mabavu.

Ayatullah Khamenei aidha amekumbusha jinai mbili za wiki iliyopita za utawala wa Aal Saud nchini Yemen ambapo shambulio la kwanza lililenga hospitali na la pili kushambulia basi lililokuwa limebeba watoto wadogo wa Yemen na kuua kwa umati makumi ya watoto wasio na hatia na kubainisha kwamba, dhamira za walimwenguni zimetikisika na kuguswa mno na jinai hizo, lakini Wamarekani badala ya kuzilaani, wamezungumzia bila ya haya uhusiano wao wa kiistratejia na utawala wa Aal Saud. Ameongeza kuwa, hali hiyo imepelekea watu kujiuliza hivi, Je! viongozi wa Marekani ni binadamu kweli?

/3738126

captcha