IQNA

Qarii mashuhuri wa Misri aaga dunia

22:18 - August 17, 2018
Habari ID: 3471630
TEHRAN (IQNA)- Qarii mashuhuri wa Misri, Sheikh Mahmoud Ismail Sharif, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 75.

Gazeti la Al Watan la Misri limemnukulu mwanae wa kiume akisema Sheikh Sharif aliaga dunia Jumanne usiku.
Alizaliwa mwaka 1943 katika eneo la Kafr Saqao katika jimbo la Sharqiya la Misri na alianza kujifunza Qur'ani utotoni na kisha akapata umaarufu kutoka na na qiraa yake iliyokuwa na mvuto.
Alijiunga na Radio ya Kitaifa ya Misri mwaka 1979 kama qarii rasmi na pia alikuwa qarii wa Sala za Ijumaa, hafla za kisiasa na mijimuiko mbali mbali kote Misri.
Marhum Sheikh Shariff pia alipata taufiki ya kualikwa katika nchi mbali mbali za dunia kusoma Qur'ani hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mazishi ya mwendazake yalifanyika katika eneo alikozaliwa Jumatano.
Misri ina umaarufu kutokana na wasomaji wake watajika wa Qur'ani ambapo aliyepata umaarufu zaidi ni Marhum Sheikh Abdul-Basit 'Abdel-Samad aliyeaga dunia mwaka 1988.Qarii mashuhuri wa Misri aaga dunia

3738716/

captcha