IQNA

Kumbukumbu ya wanadiplomasia wanne wa Iran waliotokwa nyara na Israel mwaka 1982 nchini Lebanon

18:49 - July 04, 2020
Habari ID: 3472928
TEHRAN (IQNA) - Miaka 38 iliyopita kulijiri tukio la kutekwa nyara wanadiplomasia wanne wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Lebanon.

Sayyid Muhsin Mousavi Naibu Balozi, Ahmad Mutevaselian Mwambata wa Kijeshi katika ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Taqi Rastegar Moghadam Mshauri wa Masuala ya Ufundi wa ubalozi wa Iran huko Beirut pamoja na Kadhem Akhavan ripota wa shirika la habari la IRNA walitekwa nyara na vibaraka wa utawala wa Kizayuni tarehe 5 Julai mwaka 1982 wakiwa katika kituo cha upekuzi  kaskazini mwa Lebanon.   

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran jana Ijumaa ilitoa taarifa kwa mnasaba wa tukio hilo na kueleza kuwa: "Kama ilivyotangazwa katika miaka yote hii ni kwamba ushahidi na taarifa za kuaminikia zinaeleza kuwa wanadiplomasia hao waliotekwa nyara huko Lebanon walikabidhiwa kwa wanajeshi ghasibu wa utawala wa Kizayuni na kisha wakapelekwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu; na sasa wanashikiliwa katika jela haramu za utawala huo."

Taarifa na ushahidi wa kuaminika kuhusiana na tukio hilo la kigaidi zinaonyesha kuwa wanamgambo waliokuwa wakiongozwa na Elie Hobeika na kisha Samir Geagea kutoka katika kambi za Wazayuni huko Lebanon walihusika katika utekaji nyara huo. Aidha baada ya kutekwa nyara wanadiplomasia hao wa Kiirani walipelekwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na watu hao hao na kukabidhiwa mikononi mwa idara husika za Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad).  

Kwa kuzingatia ushahidi na nyaraka za kuaminika; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajukumika kisiasa na kisheria kufuatilia utekaji nyara huo, na inaamini kuwa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake ndio wahusika wakuu wa kitendo hicho cha kigaidi. Iran inautaka pia Umoja wa Mataifa utekeleze majukumu yake ipasavyo bila ya kuingiza siasa katika suala hilo. 

3908385

captcha