IQNA

Uamuzi wa Morocco kufungua misikiti wiki ijayo

10:59 - July 09, 2020
Habari ID: 3472945
TEHRAN (IQNA) – Misikiti itaanza kufunguliwa tena nchini Morocco kuanzia Julai 15 baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa ili kuzuia kuenea kwa kasi ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco, uamuzi huo umechukuliwa baada ya wachunguzi kutathmini hali ya mambo. Aidha taarifa hiyo imesema misikiti yote itawajibika kuzingatia kanuni za afya zilizowekwa kuzuia kuenea corona.

Hatahivyo, swala za Ijumaa bado ni marufuku kwa sasa huku waumini ambao wanashukiwa kuwa na corona wakihimizwa wasifike misikitini.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco imesisitiza kuwa waumini wanatakiwa wazingatia kanuni za afya msikitini ikiwa ni pamoja na kutokaribiana na kuvaa barakoa. Aidha waumini wametakiwa wasijikusanya makundi makundi kabla na baada ya swala huku pia wakitakiwa wasipeana mkono.

Hadi sasa watu 14,771 wameambukizwa corona nchini Morocco huku wengine 242 wakifarikia dunia na waliopona ni 11,316.

3471931

captcha