IQNA

Wayemen milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa

18:36 - July 11, 2020
Habari ID: 3472950
TEHRAN (IQNA) – Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema Wayemen wasiopungua milioni 10 wa Yemen wanaandamwa na ubaha mkubwa wa chakula na hivyo wanahitaji misaada ya dharura ili kuzuia baa la njaa.

Katika taarifa, Ijumaa, WFP imesema linahitaji dola milioni 737 kufikia mwishoni mwa mwaka huu, ili kukabiliana na baa la njaa linaloisumbua nchi hiyo ya Kiarabu.

Elisabeth Byrs, msemaji wa WFP amesema hayo katika mkutano uliofanyika mjini Geneva na kuongeza kuwa, mgogoro wa kibinadamu nchini humo upo katika hali ya kutisha.

Amesema dunia inapaswa kuchukua hatua za dharura haraka iwezekanavyo na kwamba hatari ya njaa inaikabili zaidi ya asilimia 80 ya watu wote wa jamii ya nchi hiyo. 

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. 

Kituo cha Haki za Binadamu cha Ainul Insaniya kutoa ripoti na kutangaza kuwa, tokea muungano wa Saudia uanzishe vita dhidi ya Yemen mnamo Machi 26, 2015 hadi sasa, watu 16, 672 wamepoteza maisha moja kwa moja kutokana na vita hivyo na miongoni mwao kuna watoto 3,742 na wanawake 2,364.

Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3471948

captcha