Ujumbe wa Nairuzi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kwa wananchi wa Iran kwa mnasaba wa kuingia mwaka mpya wa 1393 Hijria Shamsia na kuuita mwaka huo kwa jina la mwaka wa "Uchumi na Utamaduni wenye Azma ya Kitaifa na Uongozi wa Kijihadi."
2014 Mar 21 , 22:15
Sambamba na majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuendeleza migogoro katika ardhi za Palestina kwa kuushambulia Msikiti wa kihistoria wa al Aqsa, Uri Ariel Waziri wa Makazi wa utawala huo ghasibu ameukoleza zaidi mgogoro huo kwa kuingia ndani ya msikiti mtakatifu wa al Aqswa.
2014 Mar 17 , 13:33
Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limelalamikia hatua ya banki moja ya nchi hiyo ya kuzifunga akaunti za fedha za Waislamu. Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani sambamba na kulalamikia hatua hiyo ya Tawi la Banki ya Minessota limewataka maafisa wa benki hiyo kutoa maelezo kuhusiana na hatua hiyo isiyokubalika.
2014 Mar 09 , 06:57
Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema karibu Waislamu wote waliokuwa wakiishi mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, wamelazimika kuondoka mjini humo kutokana na jinai za magaidi wa Kiksristo.
2014 Mar 09 , 06:50
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya mauaji ya umati yanayofanyika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati dhidi ya Waislamu. Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amebainisha masikitiko yake kuwa makundi ya Wakristo wenye misimamo mikali wameachwa kuendelea na mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya Kiafrika.
2014 Feb 28 , 22:10
Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC imetoa taarifa na kulaani hujuma ya hivi karibuni ya kundi la kigaidi la Boko Haram dhidi ya shule moja nchini Nigeria ambapo wanafunzi 57 waliuawa.
2014 Feb 28 , 22:04
Magaidi wa Kikristo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wamewapa Waislamu waliookwenda kujisitiri katika kanisa moja nchini humo kuondoka nchini humo au wauawe.
2014 Feb 25 , 20:35
Kamati ya Kufuta Ubaguzi ya Umoja wa Mataifa imeikosoa serikali ya Brussels kutokana na mwenendo wake wa kinyonga katika kuanzisha taasisi ya kitaifa ya haki za binadamu.
2014 Feb 25 , 20:30
Mbunge mmoja wa Chad amesisitiza kuhusu ulazima wa kutuma askari wa kimataifa kulinda maisha ya Waislamu Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mohammad Ibn Zain ameongeza kuwa kuendelea mauaji ya umati ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ni natija ya kimya cha jamii ya kimataifa.
2014 Feb 24 , 11:26
Spika wa Bunge la Uganda ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuzingatia zaidi suala la malezi ya vijana hasa wale ambao wanajihusisha na shughuli za kisayansi na kiufundi.
2014 Feb 20 , 20:43
Kundi la kutetea haki za binadamu la Palestina limetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umepiga marufuku adhana katika jela zake wanakoshikiliwa maelfu ya Waislamu wa Kipalestina.
2014 Feb 19 , 12:50
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema madola yanayoingilia masuala ya ndani ya nchi nyengine ni kikwazo kwa maendeleo na kujitawala nchi za eneo hili.
2014 Feb 09 , 11:25
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema sera za hekima za viongozi wa nchi za Mashariki ya Kati ni jambo litakalodhamini maslahi ya mataifa ya eneo.
2014 Feb 09 , 11:23