Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain amesema kuwa suala la kubadilishwa utawala wa kifalme wa nchi hiyo ndio takwa kuu la wananchi na ameutahadharisha utawala wa Aal Khalifa juu ya kupuuza matakwa ya wananchi.
2011 Aug 06 , 16:20
Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu la Ufaransa (CFCM) Muhammad Mussawi amewataka Waislamu wa nchi hiyo kuonyesha mshikamano wao na wananchi walioathiriwa na baa la njaa wa Somalia.
2011 Aug 02 , 15:50
Mchambuzi wa kisiasa wa Misri:
Baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu wanafanya jitihada kubwa za kuzuia kesi inayomkabili dikteta wa zamani wa Misri Hosni Mubarak kwani wanaelewa vyema kwamba kufikishwa mahakamani kiongozi huyo aliyeng'olewa madarakani kutawashajiisha zaidi wananchi wa nchi za eneo hili kufanya mapinduzi zaidi na kuwapandisha kizimbani viongozi vibaraka.
2011 Aug 02 , 15:21
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa msaada wa Riali milioni mia mbili kwa ajili ya watu walioathiriwa na baa la njaa nchini Somalia.
2011 Aug 01 , 13:02
Wanasheria na wanazuoni wa kidini nchini Saudi Arabia wamelaani hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kupasisha sheria ya kupambana na ugaidi inayolenga kukandamiza wapinzani wa kisiasa.
2011 Jul 31 , 12:02
Katibu Mkuu wa Jumuisya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Ekmeleddin Ihsanoglu amezitaka jumuiya za kimataifa kupambana na makundi yenye misimamo mikali barani Ulaya.
2011 Jul 31 , 10:58
Waziri Mkuu wa Norway Jens Stoltenberg ametembelea Msikiti wa Oslo ikiwa ni katika kuwajulia hali Waislamu baada ya mashambulizi ya kigaidi ya wiki iliyopita ambayo yalisababisha vifo vya makumi ya watu nchini humo.
2011 Jul 30 , 18:58
Jumuiya ya Misaada ya Kiislamu ya Ufaransa (Secours Islamique France) imeazimia kutekeleza mpango wa 'Ramadhani 2011' katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Senegal.
2011 Jul 27 , 18:51
Umoja wa Falme za Kiarabu umewakaribisha wanazuoni 35 wa Kiislamu kutoka nchi 10 kutoa mawaidha nchini humo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2011 Jul 25 , 19:05
Jumuiya ya British Health Foundation imechapisha kitabu cha Mwongozo wa wagonjwa wa kisukari wanaofunga Ramadhani.
2011 Jul 25 , 15:56
Duru za kuaminika zimeripoti kuwa Waziri Mkuu wa Bahrain akishirikiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo ameunda kundi la kigaidi kwa ajili ya kufanya mauaji dhidi ya viongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaopinga utawala wa kifalme wa nchi hiyo.
2011 Jul 23 , 17:41
Mkutano wa Kimataifa wa Dunia ya Kiislamu, Matatizo na Ufumbuzi Wake unafunguliwa leo katika mji mtakatifu wa Makka. Mkutano huo unasimamiwa na Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu.
2011 Jul 23 , 11:12
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu amewaalika maulamaa wa Kiislamu wa Iran kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa 'Ulimwengu wa Kiislamu, Matatizo na Ufumbuzi Wake' uliopangwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Makka.
2011 Jul 20 , 20:53