IQNA

Mkutano wa mwamko wa Kiislamu wafanyika Iran kujadili nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano na Israel

14:27 - September 17, 2020
Habari ID: 3473177
TEHRAN (IQNA) - Mkutano wa 13 wa Baraza la Kimataifa la Mwamko wa Kiislamu umefanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran kwa lengo la kujadil namna nchi kadhaa za Kiarabu zilivyowasaliti Wapalestina kwa kuanzisha uhusiano na utawala dhalimu wa Israel unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.

Mkutano huo umeitishwa mwa ombi la wasomi na wanachuoni wa Kiislamu na umefanyika kwa njia ya video.

Dk. Ali Akbar Velayati, Katibu Mkuu wa Baraza la Kimataifa la Mwamko wa Kiislamu amesema kuhusu sababu za kuitishwa kikao hicho cha dharura kwamba ni pamoja na baraza hilo kuhisi ni jukumu lake kukabiliana na njama zilizoongezeka hivi sasa za kujaribu kusahaulisha malengo matukufu ya Palestina. 

Kutangaza uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni kwa hakika ni usaliti wa wazi kwa malengo matukufu ya Palestina na ya Quds Tukufu na vile vile ni kuvunja makubaliano yaliyofikiwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mwaka 1946.

Utawala mtenda jinai wa Kizayuni ambao umepandikizwa katika kitovu cha ulimwengu wa Kiislamu kwa jinai, uporaji na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Waislamu, hauwezi kupata uhalali wa aina yoyote ile hata kukifanyika njama za kila namna.

Huu ni uhakika wa kihistoria na kisiasa ambao hauwezi kubadilishwa na mpango na mapatano ya aina yoyote yale. Mwezi Januari 2019, rais wa Marekani, Donald Trump alitoa pendekezo la kishetani la eti "Muamala wa Karne." Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni aliposhiriki kwenye sherehe za uzinduzi wa mpango huo aliwaambia mabalozi wa nchi tatu za Kiarabu waliohudhuria uzinduzi huo ambazo ni Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Oman kwamba ni jambo la kufurahisha sana kuona kuwa mumehudhuria sherehe hizi, kuhudhuria kwenu huku kumetoa ujumbe muhimu sana.

Sasa hivi mchakato huo wa mapatano unaendelea, na baada ya rais wa Marekani kutangaza tarehe 13 Agosti kwamba Imarati na utawala wa Kizayuni zimeweka uhusiano wa kawaida baina yao, katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja, yaani tarehe 11 Septemba, Trump ametangaza tena kwamba Bahrain nayo imeweka uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.

Watawala wa nchi za Kiarabu kama UAE, Saudi Arabia na Bahrain na nchi nyingine yoyote ya Kiarabu au ya Kiislamu ambao wana ndoto ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wanapaswa kutambua kwamba, kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu na katili ambao kwa zaidi ya miaka 70 sasa unakanyaga haki za Wapalestina na ambao hauelewi lugha yoyote isipokuwa ya mtutu wa bunduki, si tu ni kwa madhara ya wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina bali pia kunazifanya nchi hizo za Kiarabu ziwe washiriki wa jinai na uhalifu wa Wazayuni wanaomwaga damu za mamia ya maelfu ya Wapalestina.

3923446

captcha