IQNA

Shahidi Soleimani

Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Fikra za Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani

11:18 - January 06, 2023
Habari ID: 3476363
TEHRAN (IQNA)-Kongamano la Kwanza wa Kimataifa wa Fikra za Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani limemalizika hapa mjini Tehran.

Mkutano huo wa kimataifa uliofanyika kwa anuani ya "Madrassa (Fikra) ya Shahidi Soleimani" na ambao umefanyika kwa mnasaba wa mwaka wa tatu tangu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ulihudhuriwa na shakhsia, wanafikra na wasomi wa ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa yaliyokuwa malengo ya mkutano huo ni kueneza na kulinda utamaduni wa kujitolea na muqawama dhidi ya kambi ya ubeberu wa kimataifa.

Shakhsia na wasomi waliohutubia katika mkutano huo wa kwanza wa kimataifa kuhusu Shahidi Qassem Soleimani walibainisha umuhimu wa muqawama na kusimama kidete kwa ajili ya kukabiliana na madola ya kibeberu yakiongozwa na Mraekani.

Lt. Jenerali Soleimani, ambaye wakati akiuawa shahidi alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, na wanamapambano wenzao waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema  Januari 3, 2020. Shahidi Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Ikulu ya White House na Pentagon ilitangaza kuwa ilihusika na mauaji hayo ya kigaidi  na kuthibitisha kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump.

4112458/

captcha