Kwa mujibu wa IQNA, Yunus Shahmoradi, mshindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Saudia ya Attarul Kalam, ambaye alikuwepo katika Hija ya mwaka huu na waandaji wa hafla hii, aliguswa na kudhalilishwa kwa Qur'ani Tukufu.
Kijana huyu msomaji wa nchi yetu, alipokuwa akihudhuria Msikiti wa Mtume Muhammad SAW, Al Masjid An Nabawi alisoma Aya ya 32 ya Surah Tauba,ikiwa ni jibu kwa kitendo hiki cha kichaa cha raia wa Uswidi.