IQNA

Nidhamu Katika Qur'ani /6

Mikakati ya Qur'ani Tukufu kuhusu Nidhamu ya Kihisia

14:40 - April 27, 2024
Habari ID: 3478743
IQNA - Ili kutusaidia kupanga hisia zetu na kuboresha nidhamu yetu ya kihisia, Qur'an Tukufu inawasilisha mikakati au stratijia zinazoweza kutumika.

Stratijia hizo ni pamoja na kumtii Mwenyezi Mungu na kumwabudu kwa msingi wa uwiano kati ya Khawf (khofu) na Raja (matumaini).

Baada ya kutuhimiza kuunda imani thabiti na kupata msukumo wa kupanga hisia zetu, Qur'ani Tukufu inatoa mfululizo wa hatua za kuanzisha nidhamu ya kihisia. Moja ya hatua muhimu zaidi kati ya hizi ni kutii amri za Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata mwongozo wake kunahakikisha kuondolewa kwa khofu na huzuni: “Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. (Aya ya 38 ya Surah Al-Baqarah)

Qur'ani Tukufu pia inatupa mikakati ya kupanga hisia zetu na kuziachilia.. Mojawapo ya mbinu za kukabiliana na hisia hasi ni kumwabudu Mungu: "…Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema." (Aya ya 56 ya Surah Al-Aaraf)

Mtu anapomwabudu Mwenyezi Mungu, anazungumza kuhusu mahitaji yake na khofu na kumwomba kutimiza mahitaji na kuondoa khofu. Pia anatumainia rehema na baraka za kimungu. Uangalifu huu kwa pande mbili za hisia (khofu na tumaini) hujenga usawa wa kihisia na hutuweka kwenye njia ya usawa katika uhusiano wetu na Mungu na wengine.

Qur'ani Tukufu pia inatuhimiza kuepuka kujishughulisha na maisha haya ya dunia ya muda mfupi na starehe zake zinazopita: “Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo." (Aya ya 26 ya Surah Ar-Raad)

Imani hiyo hutuzuia tusiwe na furaha kupita kiasi na anasa za kilimwengu na hutusaidia kupata udhibiti zaidi juu ya hisia zetu. Kwa hakika, tunatambua kwamba njia ya kuelekea kwenye furaha na saada ya kweli ni ile inayoegemezwa kwenye baraka na rehema za Mwenyezi Mungu, sio juu ya starehe za muda za kidunia: “(Muhammad), waambie, ‘ Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.” (Aya ya 58 ya Sura Yunus).

Hivyo, kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, njia ya kuachilia aina zote za hisia ni kupitia uhusiano na Mwenyezi Mungu. Kama vile furaha inavyopaswa kuegemezwa kwenye baraka na rehema za Mwenyezi Mungu, hisia hasi zinapaswa kuachiliwa kupitia kumwabudu Mungu kwa msingi wa Khawf na Raja.

3488015

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu
captcha