Sherehe za kuadhimisha uzawa wa Imam Ali (as) zimepangwa kufanyika Juni Nne inayosadifiana na tarehe 13 Rajab katika Kituo cha Kiislamu huko London nchini Uingereza.
2012 May 15 , 18:27
Mashia wa Brazil wamesherehekea uzawa wa Bibi Mtukufu Fatma Zahra (as) katika shule pekee ya Kishia katika mji wa Sao Paulo.
2012 May 15 , 18:27
Mkutano wa Qur'ani na Ahlul Bait utafanyika tarehe 18 Mei katika mji wa Faisalabad nchini Pakistan chini ya usimamizi wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan.
2012 May 09 , 17:52
Husseiniya ya Kwanza ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Misri imefunguliwa mjini Cairo kwa kuhudhuriwa na Sheikh Ali Kurani, mwanazuoni mashuhuri wa Lebanon, ambaye amekuwa akiishi kwa miaka mingi katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
2012 May 08 , 13:50
Kundi la Kiwahabi lenye kufurutu mipaka linaloungwa mkono na Saudi Arabia na Bahrain ndilo linalosababisha mauaji ya kinyama ya Waislamu Mashia huko Pakistan.
2012 May 07 , 23:08
Waislamu nchini Uingereza wamepinga vikali pendekezo la kupigwa marufuku uchinjaji kwa njia halali ya Kiislamu.
2012 May 06 , 23:53
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amewataka wananchi wa Iran kukabiliana na njama za adui kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.
2012 Apr 30 , 08:57
Kituo cha Habari cha Kiislamu cha mji wa Toronto nchini Canada kimeanza kampeni ya kuwalingania wananchi dini ya Kiislamu kwa kutundika mabango mbalimbali yanayoarifisha dini hiyo.
2012 Apr 18 , 21:53
Chama cha al Wifaq Bahrain:
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq nchini Bahrain amekemea misimamo ya kindumakuwili ya jamii ya kimataifa kuhusu mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo na kusema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuwa pamoja na wananchi na si pamoja na madikteta.
2012 Apr 18 , 21:53
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa serikali ya Bahrain kuheshimu haki za wananchi wa nchi hiyo na kuwaruhusu kuandamana kwa amani.
2012 Apr 17 , 21:21
Mgombea wa kiti cha rais aliyekataliwa na Kamisheni Kuu ya Uchaguzi ya Misri kheirat al Shater amewasilisha malalamiko yake kwa kamisheni hiyo.
2012 Apr 16 , 23:58
Masomo ya Uislamu na Ufanisi wa Mwanadamu kwa ajili ya watu walioingia katika dini tukufu ya Kiislamu yamemalizika katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.
2012 Apr 16 , 23:58
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo Jumapili amehutubia hadhara iliyojumuisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah), makamanda wa jeshi la polisi na wafanyakazi wa jeshi hilo na kusisitiza kuwa kuwaridhisha wananchi humfanya mwanadamu apate radhi za Mwenyezi Mungu.
2012 Apr 16 , 00:25