Maelfu ya wananchi wa Tunisia wameandamana wakitaka kuundwa serikali ya Kiislamu nchini mwao.
2012 Mar 26 , 12:43
Wakristo wa mji wa New York nchini Marekani walifanya maandamano jana wakipinga kitendo cha watu wasiomwamini Mungu cha kukana kuwepo Mwenyezi Mungu Mtukufu.
2012 Mar 25 , 12:13
Washiriki katika kikao cha viongozi wa kidini nchini Ufaransa wametoa taarifa wakilaani vitendo vya baadhi ya wagombea urais wa nchi hiyo vya kutumia vibaya masuala ya kidini katika kampenzi zao. taarifa hiyo imetiwa saini na viongozi wa dini za Kikristo, Uislamu, Uyahudi na Budha.
2012 Mar 18 , 16:25
Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kimetoa taarifa kikilaani shambulizi lililofanywa dhidi ya Msikiti wa Imam Ridha (as) katika mji mkuu wa Ubelgiji huko Brussels na kumuua shahidi Imam wa msikiti huo.
2012 Mar 17 , 19:00
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo Jumanne amekutana na wafanyakazi wa Jumuiya ya Wakfu na Masuala ya Kheri ya Iran na kusisitiza kuwa wakfu ni taasisi bora ya kidini na kwamba kuna udharura wa kuenezwa zaidi suna hiyo ya kutoa wakfu katika jamii kwa kuwahamasisha watu kufanya amali hiyo na kutekeleza kwa njia sahihi haki za watu wanaotoa wakfu.
2012 Mar 13 , 19:10
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amekagua Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Mafuta na kuona kwa karibu shughuli zinazofanyika katika kituo hicho.
2012 Mar 12 , 22:23
Kongamano la pili la Waislamu Nchini Marekani limepangwa kufanyika tarehe 22 na 23 Septemba mwaka huu katika Chuo Kikuu cha DePaul katika mji wa Chicago.
2012 Mar 11 , 14:59
Jumuiya ya Kiislamu ya Kielimu, Kisayansi na Kiutamaduni ISESCO imetuma ujumbe kwa nchi zote za ulimwengu wa Kiislamu kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambaye huadhimishwa Machi nane kila mwaka.
2012 Mar 06 , 12:49
Idadi ya Misikiti nchini Marekani imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha muongo moja uliopita pamoja na kuwepo vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu baada ya matukio ya 9/11.
2012 Mar 03 , 17:59
Msikiti wa kihistoria wa Quba ambao ni wa kwanza kabisa kujengwa na Waislamu ulioko katika mji mtakatifu wa Madina, utafanyiwa ukarabati na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia.
2012 Feb 21 , 18:30
Mwandishi wa kisalafi wa Kuwait Muhammad al Malifi aliyemvunjia heshima Imam wa Zama Mahdi (as) amewekwa korokoroni.
2012 Feb 20 , 14:16
Benki ya kwanza ya Kiislamu ilifunguliwa rasmi jana nchini Nigeria baada ya miezi kadhaa ya mjadala na mazungumzo na serikali ya nchi hiyo.
2012 Feb 19 , 11:37
Sheikh wa al Azhar ameafiki suala la kukatwa misaada ya kifedha ya Marekani kwa Misri ikiwa ni ishara ya kupinga uingiliaji wa serikali ya Washington katika masuala ya ndani ya Misri.
2012 Feb 18 , 18:59