Sheikh wa al Azhar ameafiki suala la kukatwa misaada ya kifedha ya Marekani kwa Misri ikiwa ni ishara ya kupinga uingiliaji wa serikali ya Washington katika masuala ya ndani ya Misri.
2012 Feb 18 , 18:59
Kongamano la Kimataifa la 'Utambulisho wa Kiislamu na Utandawazi' litafanyika Tehran katika Chuo Kikuu cha Tarbiat Modaress.
2012 Feb 18 , 16:31
Ayatullah Ali Khamenei ameitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mama wa mwamko wa Kiislamu wa Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika na kusema utawala wa Kiislamu wa Iran umo katika harakati ya kuelekea kwenye utambulisho halisi, wenye kudumu, imara na unaoweza kutetewa mbele ya hujuma mbalimbali.
2012 Feb 08 , 21:41
Kikao cha pili cha Mwamko wa Kiislamu, Mwangwi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kinafanyika leo Jumatatu katika Husainiya ya al Zahra (as) ya Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu mjini Tehran.
2012 Feb 06 , 16:25
Waislamu nchini Afghansitan wameanzisha Taasisi ya Al Mahdi (ATF) kwa lengo la kueneza mafundisho ya Kiislamu, utamaduni wa kidini na kuandaa mazingira ya Umoja wa Kiislamu.
2012 Feb 04 , 14:35
Semina iliyopewa jina la "Sauti za Qur'ani Tukufu, Kutafuta Rehma Ndani ya Qur'ani" imepangwa kufanyika tarehe 14 Februari katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.
2012 Feb 01 , 20:14
Kongamano la Mapinduzi ya Tunisia katika Mtazamo wa Sira ya Mtume (saw) limepangwa kuanza kesho tarehe 2 hadi 3 Februari katika mji wa Qairawan nchini Tunisia.
2012 Feb 01 , 20:14
Muislamu mmoja huko Ujerumani ameanzisha tovuti ya huduma ya taxi za Waislamu ambapo Wajerumani wanaweza kusafiria katika magari ya jinsia moja, tovuti ya thelocal.de imeripoti.
2012 Jan 31 , 13:26
Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza kimeandaa kongamano la 'Vituo vya Elimu na Mabadiliko katika Jamii za Waislamu' ambalo litafanyika chuoni hapo 27-28 Agosti mwaka huu wa 2012.
2012 Jan 31 , 13:20
Kamanda anayesimamia masuala ya usalama katika mji mtakatifu wa Samarra nchini Iraq ametangaza habari za kutekelezwa operesheni maalumu za kiusalama katika mji huo kwa mnasaba wa kuwadia maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hassan Askari (as) hapo siku ya Jumatano Februari Mosi.
2012 Jan 29 , 16:18
Mkutano wa kitaifa wa "Maulidi Mwaka 2012" utafanyika nchini Ufaransa tarehe 11 Februari kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa mbora wa viumbe, Mtume Muhammad bin Abdullah (saw).
2012 Jan 29 , 10:23
Maandamano ya kwanza ya vyombo vya habari kwa lengo la kuunga mkono Quds Tukufu yatafanyika Ijumaa Machi pili.
2012 Jan 28 , 16:30
Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania amewataka maulamaa wa Kiislamu kutoa mchango katika marekebisho ya jamii na kuonesha njia halisi ya Uislamu kwa wananchi.
2012 Jan 23 , 17:31