Serikali ya jimbo la Cuebec nchini Canada imetoa taarifa likilaani mashambulizi yaliyofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya msikiti wa mji wa Gatino.
2012 Jan 08 , 17:07
Kituo cha Kiislamu cha al Azhar kimetangaza kuwa kinapinga Taasisi ya Kuamrisha Mema iliyoanzishwa nchini Misri kwa kuiga Mawahabi wa Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, kuanzishwa kwa chombo hicho kunapingana na uwepo wa al Azhar ambayo ndio marejeo pekee ya kisheria ya kutoa hukumu za kidini nchini Misri.
2012 Jan 07 , 17:02
Mkutano maalumu wa vijana Waislamu nchini Uhispania umefanyika katika Msikiti Mkuu wa Madrid.
2012 Jan 07 , 14:18
Kikao cha dharura cha kuchunguza sheria ya kuratibu upya Kituo cha Kiislamu cha al Azhar kilifanyika jana chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar mjini Cairo.
2012 Jan 05 , 12:19
Muungano wa "Watu Huru wa Qatif" umetoa taarifa ukiitangaza Ijuma ijayo kuwa ni "Siku ya Zilzala ya Watu Huru" na umetoa wito wa kufanyika maandamano makubwa dhidi ya hukumu ya kutiwa nguvuni Waislamu 23 wa madhehebu ya Shia nchini humo.
2012 Jan 04 , 20:10
Mwendesha mashtaka wa mkoa wa Asyut wa Misri amemhukumu kifungo cha siku nne jela Jamal Abduh Mas'ud, Mkristo wa Kikopti aliyepatikana na hatia ya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) katika mtandano wa kijamii wa Facebook.
2012 Jan 01 , 15:17
Wimbi la mwamko wa Kiislamu limetoa fursa bora zaidi ya kufikiwa lengo la kuyakurubisha madhehebu ya Kiislamu, amesema mwanazuoni wa umoja wa Kiislamu nchini Iran.
2012 Jan 01 , 11:24
Taifa la Iran Ijumaa tarehe 30 liliadhimisha mwaka wa pili wa Hamasa ya Tisa Dey. Katika miongo mitatu tokea ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu, kumekuwepo na siku muhimu na zenye taathira kubwa katika kuendeleza harakati ya kimapinduzi ya taifa la Iran. Hamasa ya Tisa Dey ni kati ya siku hizo muhimu.
2012 Jan 01 , 11:20
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema Wamagharibi wana hofu na woga kutokana na mabadiliko yanayojiri sasa katika eneo la Mashariki ya Kati hususan muungamo wa mataifa ya Kiislamu.
2011 Dec 31 , 00:21
Wakati mwanadamu anapomtegemea Mwenyezi Mungu, huweza kufikia utulivu wa moyoni, amesema Sheikh Mohammad Abbaspour mwanasaikolojia mwandamizi nchini Iran.
2011 Dec 29 , 16:58
Mkutano wa "Waislamu katika Jamii Zisizo za Kiislamu" utafanyika Jumamosi ijayo katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.
2011 Dec 25 , 14:59
Wanazuoni na wanafunzi wa chuo cha kidini cha al-Azhar nchini Misri jana Ijumaa waliandamana katika uwanja wa Tahrir kulaani siasa za ukandamiza za Baraza la Kijeshi linaloongoza nchi hiyo.
2011 Dec 24 , 16:05
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO jana Ijumaa lilitoa taarifa likilaani mashambulio yaliyofanywa hivi karibuni na magaidi mjini Baghdad, Iraq.
2011 Dec 24 , 16:05