Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO jana Ijumaa lilitoa taarifa likilaani mashambulio yaliyofanywa hivi karibuni na magaidi mjini Baghdad, Iraq.
2011 Dec 24 , 16:05
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amekutana na Mwenyekiti wa chama cha Ukombozi wa Kitaifa ambapo pande hizo mbili zimechunguza hali ya ndani na eneo la Mashariki ya Kati.
2011 Dec 21 , 18:57
Wapalestina wanaoishi katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu na Wazayuni mwaka 1948 walifanya maandamano jana wakipinga rasimu iliyowasilishwa katika Bunge la Israel ya sheria ya kupingwa marufuku adhana katika misikiti ya Waislamu.
2011 Dec 18 , 12:54
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetoa taarifa ikilaani shambulizi lililofanywa na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Msikiti wa al Nour katika Ukingo wa Magharibi.
2011 Dec 17 , 18:55
Kituo cha Alwaleed Cha Utafiti wa Uislamu katika Dunia ya Leo katika Chuo Kikuu cha Edinburg kimeandaa kongamano la ‘Waislamu na Ushiriki wa Kisiasa Nchini Uingereza’ kuanzia Aprili 20-21 mwaka 2012.
2011 Dec 14 , 16:24
Wanafikra na wasomi wa Kiislamu na Kikristo wanakutana leo Jumanne mjini Paris, Ufaransa kwa madhumuni ya kuchunguza mipaka na pande mbalimbali za mazungumzo baina ya dini za mbinguni.
2011 Dec 13 , 14:32
Naibu Mwenyekiti wa chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri Isam al Aryan amesema kuwa ushindi wa wanaharakati wa Kiislamu katika chaguzi za kwanza huru katika nchi za Misri na Tunisia ni kielelezo kwamba mapinduzi yaliyofanyika katika nchi hizo ni ya Kiislamu.
2011 Dec 12 , 13:25
Kongamano la 'Uislamu wa Kifaransa' au 'Uislamu Nchini Ufaransa' limepangwa kufanyika Jumamosi ijayo ya tarehe 17 Disemba katika mji wa Marseille.
2011 Dec 12 , 11:45
Daktari mmoja Muislamu ameanzisha zahanati inayotoa huduma za tiba bure na bila ya malipo kwa watu wenye haja katika jimbo la Carolina kwa lengo la kudhihirisha sura halisi ya Uislamu.
2011 Dec 10 , 17:05
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na ujumbe wa taasisi hiyo nchini Afghanistan wamelaani milipuko ya mabomu iliyolenga Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa katika maombolezo ya kifo cha Imam Hussein (as) katika miji ya Kabul na Mazar Sharif na kuua makumi ya raia wasiokuwa na hatia yoyote.
2011 Dec 08 , 12:42
Mwanachama wa kundi moja la kibaguzi la Ufaransa ambaye tarehe 10 Novemba alichoma moto Msikiti wa Montbéliard ametiwa nguvuni.
2011 Dec 08 , 12:41
Baraza la Waislamu wa Ufaransa limetoa taarifa likilaani mpango uliowasilishwa katika Baraza la Seneti la nchi hiyo wa kupiga marufuku vazi la hijabu ya Kiislamu katika vituo vya starehe na michezo na shule za chekechea.
2011 Dec 07 , 17:47
Mashia na Masuni wa India walikutana jana Jumamosi huko Srinagar, mji mkuu wa jimbo la Jamu na Kashmir ili kujadili njia za kuimarisha amani na umoja kati yao.
2011 Dec 04 , 15:17