Mashia na Masuni wa India walikutana jana Jumamosi huko Srinagar, mji mkuu wa jimbo la Jamu na Kashmir ili kujadili njia za kuimarisha amani na umoja kati yao.
2011 Dec 04 , 15:17
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeilaumu Saudi Arabia kwa kupuuza haki za Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo na kutangaza kuwa utawala wa kifalme wa Riyadh umewatia mbaroni zaidi ya Mashia 300 kwa sababu ya kushiriki katika maandamano ya amani.
2011 Dec 03 , 16:54
Matokeo ya awali na yasiyokuwa rasmi ya uchaguzi wa Bunge nchini Misri yanaonesha kwamba chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la Harakati ya Ikhwanul Muslimin kimeshinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo.
2011 Nov 30 , 17:00
Waislamu wa madhehebu ya Shia walioko Romania wakiwemo Wairani 4000 hawana misikiti, amesema mkurugenzi wa Kituo cha Fiqhi ya Aimma At’har AS.
2011 Nov 30 , 16:12
Mahakama ya Masuala ya Kiidara ya mji wa Alexandria nchini Misri imefuta na kubatilisha marufuku ya vazi la hijabu la wanawake wa Kiislamu iliyokuwa imewekwa na Waziri wa Habari wa serikali iliyong'olewa madarakani ya Hosni Mubarak.
2011 Nov 29 , 16:56
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa njama zinazofanywa na madola ya Magharibi kwa ajili ya kukandamiza na kupotosha mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni juhudi zilizogonga mwamba.
2011 Nov 28 , 00:04
Chama cha Kiislamu cha Uadilifu na Usawa cha Moroco kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana nchini humo.
2011 Nov 26 , 19:04
Mwakilishi wa Sheikh wa al Azhar nchini Misri jana alishiriki katika maandamano ya wananchi katika Medani ya Tehrir na kutangaza uungaji mkono wa kiongozi huyo wa kidini kwa wananchi wanaoandamana.
2011 Nov 26 , 19:00
Kituo kimoja cha utafiti nchini Uholanzi kimetangaza kuwa wanawake 6 kati ya kila 10 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 35 nchini humo wanatumia vazi la hijabu bila ya kizuizi chochote.
2011 Nov 23 , 20:15
Wiki ya Ujue Uislamu ilianza jana katika mji wa Batley nchini Uingereza chini ya usimamizi wa jumuiya ya IMWS ya Waislamu wa India.
2011 Nov 23 , 20:14
Polisi ya mjini wa Toronto nchini Canada imewaruhusu polisi wa kike Waislamu kutumia vazi la hijabu ya Kiislamu.
2011 Nov 23 , 20:13
Rais Giorgio Napolitano wa Italia ameitaka Vatican kutayarisha uwanja wa kufanyika mazungumzo kati ya dini mbalimbali nchini Italia.
2011 Nov 23 , 20:12
Kongamano la Kimataifa kuhusu ‘Dini na Utandawazi’ limefanyika kati ya Novemba 22-23 nchini Algeria mjini Algiers.
2011 Nov 23 , 16:41