Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amekutana na maafisa wanaoshughulikia Hija mwaka huu wa Iran akiitaja ibada hiyo kuwa ni fursa ya thamani kwa ajili ya kujenga mawasiliano na umma wa Kiislamu na kujifaidisha kimaanawi na kiroho.
2011 Oct 04 , 02:20
Duru ya nane ya kikao cha Muungano wa Wakuu wa Kodi na Masuala ya Zaka wa Nchi za Kiislamu ilifanyika jana Jumapili huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.
2011 Oct 03 , 14:46
Waziri wa Sheria wa Niger ametangaza kuwa Baraza la Taifa la Mpito la Libya linaweza kumsaili Saadi Gaddafi, mwana wa kiume wa dikteta mtoro wa Libya aliyekimbilia nchini himo.
2011 Oct 02 , 10:57
Kikao cha dharura cha Mawaziri wa Elimu ya Juu wa nchi za Kiislamu kimepangwa kufanyika tarehe 4 na 5 mjini Riyadh, Saudi Arabia.
2011 Oct 01 , 17:07
Kikao cha tatu cha Mawaziri wa Afya wa Nchi za Kiislamu kilianza siku ya Alkhamisi huko katika mji wa Astana ambao ni mji mkuu wa Kazakhstan.
2011 Oct 01 , 16:46
Sayyid Haidar al Satri ambaye ni mwanachama wa Baraza Kuu la Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain amesema kuwa ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya wanawake wanaopinga siasa za serikali ya nchi hiyo ni alama ya udhaifu wa watawala wa kifalme wa nchi hiyo.
2011 Sep 27 , 21:53
Tarehe 25 Shawwal mwaka 148 Hijria Qamaria, Ulimwengu wa Kiislamu ulitumbukia katika msiba mkubwa kutokana na kumpoteza Imam Sadiq AS kutoka Ahlul Bayt wa Mtume SA. Katika siku hii Imam Ja’afar Sadiq AS akiwa na umri wa miaka 65 alifikia daraja ya shahada baada ya kupewa sumu kwa amri ya Mansur Dawaniqi, Khalifa wa Pili wa silisili ya Makhalifa wa Bani Abbas.
2011 Sep 22 , 14:05
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei amesema kuwa mabeberu wanatumia mbinu ya kuchafua amani ya kijamii, kimaadili na kiroho kwa ajili ya kukabiliana na mataifa yanayojitawala.
2011 Sep 20 , 22:07
Askari polisi wa Bahrain wameshambulia waandamanaji waliokuwa na hasira ambao walikuwa wakilalamikia kitendo cha kuuawa shahidi kijana mmoja wa nchi hiyo aliyeteswa hadi kufa.
2011 Sep 19 , 09:36
Beshara Boutros ar- Rai, Askofu Mkuu wa Wakristo wa Kimaroni wa Lebanon ametaka kusambazwa kwa fikra za Imam Musa Sadr aliyetekwa nyara na utawala wa dikteta wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
2011 Sep 18 , 15:21
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetaka Baraza la Mpito la Libya litambuliwe kama mwakilishi rasmi wa wananchi wa nchi hiyo na kuungwa mkono.
2011 Sep 17 , 20:07
Balozi wa utawala wa kizayuni wa Israel nchini Jordan ameikimbia nchi hiyo kutokana na hofu ya maandamano makubwa dhidi ya Israel yaliyofanyika karibu na ubalozi wa utawala huo haramu mjini Amman.
2011 Sep 16 , 10:59
Sheikh Yusuf Qaradhawi Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu amechukua misimamo ya kindumakuwili kuhusu matukio yanayojiri katika ulimwengu wa Kiarabu.
2011 Sep 13 , 12:57