Sheikh Yusuf Qaradhawi Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu amechukua misimamo ya kindumakuwili kuhusu matukio yanayojiri katika ulimwengu wa Kiarabu.
2011 Sep 13 , 12:57
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa jeshi, taifa na harakati ya mapambano ya Hizbullah ni mambo yanayoipa fahari kubwa nchi hiyo.
2011 Sep 08 , 12:29
Kesi ya Firauni wa zama wa Misri dikteta Hosni Mubarak, wanawe wawili, waziri wa mambo ya ndani wa zamani na maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa masuala ya usalama imeendelea leo mjini Cairo chini ya ulinzi mkali wa polisi na askari usalama.
2011 Sep 07 , 22:56
Makala yenye anwani ya ‘Mazingira kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna’ imeandikwa na Ali Najarpourian na kuchapishwa katika toleo la 69 la jarida la Bayyenat.
2011 Sep 07 , 15:39
Imam Ali AS amesema: ‘Kina baba wana jukumu la kuwapa watoto majina yanayofaa, kuwalea vizuri na kuwafunza Qur’ani.’
2011 Sep 06 , 22:04
Katibu Mkuu wa Harakati ya Wapigania Uhuru wa Bahrain amesema kuwa utawala wa kizazi cha Aal Khalifa nchini humo utaporomoka kama zilivyoondolewa madarakani tawala za Hosni Mubarak huko Misri na Muammar Gaddafi huko Libya.
2011 Sep 06 , 14:33
Sheikh Hassan Saffar ambaye ni miongoni mwa maulamaa wakubwa wa Kishia wa Saudi Arabia amesema kuwa mashekhe wanaotoa fatuwa za kuhalalisha mauaji ya watu wasiokuwa na hatia wanashiriki pia katika umwagaji wa damu za watu hao.
2011 Sep 04 , 15:23
Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Uokovu wa Libya amesema kuwa Wamagharibi wana wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kuundwa serikali ya Kiislamu nchini humo na kusisitiza kuwa Walibya wanataka kuundwa serikali itakayosimama juu ya misingi ya sheria za Kiislamu.
2011 Sep 04 , 12:56
Ayatullah Abdul Amir Qabalan, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Mashia wa Lebanon amevitaka vyama vya kisiasa vya nchi hiyo kuimarisha umoja miongoni mwao na kufanya mazungumzo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto na vilevile kutatua matatizo ya nchi hiyo.
2011 Sep 03 , 11:58
Kiongozi Muadhamu katika Baraza la Idul Fitri:
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia hadhara ya viongozi wa serikali na matabaka mbalimbali ya wananchi katika Husainiya ya Imam Khomeini mjini Tehran akiutaja mwamko wa sasa wa Kiislamu kuwa ni harakati ya Waislamu kurejea kwenye utambulisho wao wa asili.
2011 Sep 01 , 11:03
Wananchi wa Saudi Arabia na hasa tabaka la vijana, wanafuatilia kwa karibu matatizo yanayowakabili ya kijamii na kiuchumi yakiwemo ya uhuru, umasikini na ubaguzi na jambo hilo linaweza kongeza harakati za mapinduzi nchini humo.
2011 Aug 30 , 15:07
Waislamu wa Marekani wameamua kuwakaribisha wasiokuwa Waislamu katika sikukuu ya Idul Fitr iliyopewa jina la Siku ya Milango Wazi ya Misikiti na Vituo vya Kiislamu.
2011 Aug 29 , 15:49
Ali al Adiib ambaye ni miongoni mwa maafisa wa chama cha Kiislamu cha al Daawa cha Iraq amesema kuwa Mawahabi wa Saudi Arabia wametoa fatuwa inayohalalisha mauaji dhidi ya raia wa Iraq na kueneza gaidi nchini humo.
2011 Aug 28 , 18:56