Ali al Adiib ambaye ni miongoni mwa maafisa wa chama cha Kiislamu cha al Daawa cha Iraq amesema kuwa Mawahabi wa Saudi Arabia wametoa fatuwa inayohalalisha mauaji dhidi ya raia wa Iraq na kueneza gaidi nchini humo.
2011 Aug 28 , 18:56
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa moja ya ujumbe muhimu za mwamko wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel unajitayarisha kwa ajili ya kutoweka.
2011 Aug 26 , 21:40
Kiongozi wa Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq Sayyid Ammar Hakim amewapongeza wananchi wa Libya kwa kupata ushindi dhidi ya dikteta wa nchi hiyo na kusema viongozi wa nchi za Mashariki ya Kati wanapaswa kupata ibra na funzo kutokana na hatima ya dikteta wa Libya.
2011 Aug 24 , 17:42
Huku uhusiano wa Misri na Israel ukiendelea kuharibika, kijana mmoja mwanamapinduzi wa Misri ameteremsha chini na kuichoma moto bendera ya Israel katika ubalozi wa utawala huo nchini Misri, na kuweka bendera ya Misri mahala pake.
2011 Aug 21 , 15:43
Mapinduzi yanayoendelea katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa bara la Afrika ni fursa nzuri ya kuwekwa kando tofauti za kimadhehebu na kikabila kati ya Waislamu.
2011 Aug 21 , 15:05
Kiongozi nambari mbili wa utawala wa Libya Abdulsalam Jalud amejiunga na wanamapinduzi wa nchi hiyo sambamba na tangazo la kusonga mbele zaidi wapiganaji wanaotaka kumuondoa madarakani diketa wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.
2011 Aug 20 , 16:23
Baraza la Jumuiya za Kiislamu za Iraq zilizo nchini Ujerumani limeanzishwa nchini Ujerumani. Baraza hilo limeanzishwa na Wairaqi wanaoishi nchini humo.
2011 Aug 20 , 14:46
Baraza la ugavana wa mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq limetangaza kwamba siku ya Jumatatu tarehe 21 Ramadhani inayosadifiana na tarehe 22 Agosti ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Imam Ali bin Abi Twalib (as) itakuwa siku ya mapunziko rasmi mjini humo.
2011 Aug 20 , 12:22
Kikao cha Kigezo cha Qur'ani katika Mwamko wa Kiislamu kimefanyika pambizoni mwa Maonyesho ya 19 Kimataifa ya Qur'ani yanayoendelea mjini Tehran.
2011 Aug 19 , 12:54
Mkutano wa 'Ubahai na Uzayuni' ulifanyika jana mjini Tehran katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani.
2011 Aug 19 , 12:54
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran wanatumia silaha ya vikwazo kwa shabaha ya kutoa dharba dhidi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran, lakini lengo hilo la kihasama limefeli kutokana na hima kubwa ya viongozi na wananchi.
2011 Aug 18 , 09:49
Akiashiria mabadiliko ya kisiasa ambayo yametokea katika nchi za Kiislamu na kuwepo matabaka mbalimbali ya wananchi katika mabadiliko hayo, Nilufar Bakhtiyar, mbunge wa Pakistan amesema kuwa kuwepo wanawake katika mkondo mzima wa mabadiliko hayo kunathibitisha wazi nafasi yao muhimu katika maamuzi ya mabadiliko hayo.
2011 Aug 17 , 15:03
Kikao kuhusu ‘Nafasi ya Wanawake katika Uislamu’ kimefanyika Agosti 16 katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
2011 Aug 17 , 11:59