IQNA

Uturuki Yawatunuku Waislamu wa Uhispania Nakala 3,000 za Qur’ani

13:27 - March 30, 2018
Habari ID: 3471448
TEHRAN (IQNA)-Uturuki imewatunuku Waislamu wa kusini mwa Uhispania nakala 3,000 za Qur’ani Tukufu.

Taasisi ya taasisi ya Turkiye Diyanet Foundation (TDV), ambayo inajihusisha na masuala ya Kiislamu, imesema tarjuma za Qur’ani kwa lugha ya Kihispania zimesambazwa miongoni mwa Waislamu wa maeneo ya Granada na Seville katika eneo la Andalusia kusini mwa Uhispania kama sehemu ya kampeni ya ‘Zawadi Yangu Iwe ni Qur’ani Tukufu.”

Kampeni hiyo iliyozinduliwa na TDV pamoja na Idara ya Masuala ya Kidini ya Serikali ya Uturuki (Diyanet) inalenga kusambaza nakala zaidi ya milioni moja za Qur’ani kote duniani  zikiwemo nchi za maeneo ya mbali ya Amerika ya Latini na Asia Pasifiki. Nakala hizo za Qur’ani zina lugha ya Kiarabu kando ya tarjuma ya lugha mbali mbali. Hadi sasa idara hiyo imefanikiwa kutayarisha tarjuma za Qur’ani tukufu kwa lugha 17 za maeneo mbali mbali ya dunia.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Uhispania na Ureno ni nchi zilizokuwa zinatawaliwa na Waislamu kati ya miaka 711 and 1492 Miladia wakati huo eneo hilo likijulikana kama Al-Andalus. Katika karne ya 8 na 9 polepole sehemu kubwa ya Wakristo walipokea Uislamu uliokuwa dini tawala. Mnamo mwaka 1100 takriban 80% za wakazi walikuwa Waislamu kabla ya hali kubadilika katika karne zilizofuata.

3465468

captcha