IQNA

Rais wa Ufaransa aendeleza vita dhidi ya Uislamu

11:07 - February 19, 2020
Habari ID: 3472485
TEHRAN (IQNA) - Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameendeleza vita vyake dhidi ya Uislamu baada ya kutangaza kuwa atapambana na 'Uislamu wa kisiasa."

Akizungumza Jumanne wakati alipotembelea mji wa Mulhouse kaskazini mashariki mwa Ufaransa, Macron alitangaza stratijia yake ya kupambana na 'mrengo wa Kiislamu wa wanaotaka kujitenga'.

Macron amedai kuwa katika baadhi ya maeneo ya Ufaransa hali ya kutaka kujitenga imeenea sana katika jamii na hivyo ameahidi kukabiliana na hali hiyo.  Macron ambaye anakosolewa kutokana na sera zake za kuupiga vita Uislamu amesema serikali inachunguza muundo wa Uislamu Ufaransa hasa masomo ya watoto Waislamu na ufadhili wa maeneo ya ibada hasa yale yanayopokea misaada kutoka nje ya nchi.

Safari ya Macron mjini Mulhouse ni ya kwanza katika safari ya wiki kadhaa yenye lengo la kukabiliana na kile anachosema ni Uislamu wenye misimamo ya kufurutu ada.

Hayo yanajiri wakati ambao, uchunguzi wa maoni umebaini kuwa asilimia 42 ya Waislamu Ufaransa wanabaguliwa au kubughudhiwa nchini humo.

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Maoni ya Umma Ufaransa umebaini kuwa Waislamu wanabaguliwa na kusumbuliwa bila sababu wakati wa doria ya polisi, wanapotaufta kazi na wanapokodi nyumba.

Asilimia 60 ya wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu au mtandio wanasema wamewahi kubaguliwa au kusumbuliwa kwa uchache mara moja.

Kuna takribani Waislamu milioni sita Ufaransa wengi wao wakiwa ni wahamiaji kutoka nchi za kaskazini mwa Afrika na idadi hiyo ni takribani asilimia nane ya Wafaransa wote.

3879841

captcha