IQNA

Shirika la Habari la IQNA lazindua ligha ya Kireno

19:46 - December 29, 2021
Habari ID: 3474737
TEHRAN (IQNA)- Lugha ya Kireno sasa ni lugha ya 21 katika Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA).

Uzinduzi wa IQNA kwa lugha la Kireno umefanyika Jumanne mjini Tehran katika  maonyesho ya mafanikio ya Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR)  na kuhudhuriwa na Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika vyuo vikuu Hujjatul Islam Mustafa Rostani, Mkurugenzi wa IQNA Mohammad Hossein Hassani na Mkurugenzi wa Taasisis ya  Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran. Kwa kuzinduliwa lugha ya Kireno, sasa IQNA itakuwa na lugha 21.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) ndio la kwanza na la pekee ambalo linashughulikia kwa njia maalumu habari za Quran katika ulimwengu wa Kiislamu. Shirika hili lilianzishwa Novemba 11, 2003 sawa na tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1424 Hijria Qamaria katika sherehe iliyohudhuriwa na rais wa wakati huo wa Iran.

IQNA huakisi habari za Qur'ani ambazo zinaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuleta umoja katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Lugha ya Kireno inazungumzwa na watu zaidi ya millioni 270 kote duniani na inatajwa kuwa miongoni mwa lugha 10 zenye wazungumzaji wengi zaidi duniani.

Ligha ya Kireno ni lugha rasmi Ureno, Angola, Msumbiji, Guinea-Bissau, Cape Verde, São Tomé na Príncipe, Brazil, Timor Mashariki, Equatorial Guinea, and Macau. Aidha ni miongoni mwa lugha 10 zenye wazungumzaji wengi barani Afria na ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika miongoni mwa taasisi zingine za kimataifa.

4020508

captcha