IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Nchi 25 kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran

17:54 - March 06, 2024
Habari ID: 3478458
IQNA - Waandaaji wa toleo la 2024 la Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran wanasema nchi 25 zimetangaza kuwa tayari kushiriki katika hafla hiyo.

Haya ni kwa mujibu wa Shobeir Firouzian, Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani na Etrat.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne kuhusu maonyesho hayo yajayo, alibainisha kuwa nchi 25 zikiwemo Uturuki, Algeria, Senegal, Russia, India, Ufaransa, Afrika Kusini, China na Canada zitashiriki katika hafla hiyo.

Sehemu ya kimataifa ya maonyesho hayo itafunguliwa Machi 20 na itaendeshwa kwa siku saba, aliongeza.

"Mkutano wa Qur'ani wa Tehran" pia utafanyika kando ya hafla hiyo kwa kushirikisha mawaziri wa utamaduni kutoka nchi tano za Kiislamu, alisema.

Kama maonyesho yaliyopita, maonyesho ya mwaka huu yatafanyika yenye kauli mbiu ya "Ninakusoma".

Ukumbi wa Salah (Mosallah) wa Imam Khomeini (RA) utakuwa mwenyeji wa hafla hiyo ya kimataifa ya Qur'ani kuanzia Machi 21 hadi Aprili 3.

"Moja ya sehemu muhimu na muhimu ya maonyesho ya Qur'ani mwaka huu ni sehemu ya watoto," alisema Firouzian, akibainisha kuwa "programu maalum" kama vile michezo na ukumbi wa michezo zitafanyika.

Milo rahisi ya iftar itatolewa kwa wageni, alisema.

Moja ya sehemu nyingine katika maonyesho hayo inahusisha utafiti wa Qur'ani, alisema, akiongeza kuwa kila mwaka, idadi kubwa ya wahudhuriaji huja mahsusi kwa ajili ya mashauriano yanayohusu Qur'ani. "Quran inatoa mipango na suluhisho kwa kila aina ya shida," amebaini

Maonyesho ya mwaka huu yana sehemu maarufu ya mavazi ya Iran na Kiislamu, alisema, akiongeza kuwa wazalishaji 205 watatoa bidhaa zao katika hafla hiyo.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu wa Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini Iran na katika uga wa kimataifa..

Aidha maonyesho hayo huwa kituo cha kuwasilisha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia huuzwa bidhaa mbalimbali zinazohusiana na Qur'ani.

3487442

Habari zinazohusiana
Kishikizo: maonyesho ya qurani
captcha