IQNA

Ramadhani katika Quran

Fadhila za Usiku wa Laylatul Qadr

17:43 - April 02, 2024
Habari ID: 3478617
IQNA - Usiku wa Qadr, au Laylatul Qadr unaojulikana pia kama Usiku wa Hatima, una sifa nzuri kama zilivyoangaziwa katika Qur'ani Tukufu. Fadhila hizi hutumika kuwahimiza waumini wanufaike na usiku huu ambao unapatikana katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Usiku wa Qadr ni usiku wa baraka. Kama ilivyoelezwa katika Aya ya pili na ya tatu ya Surah Ad-Dukhan, Mwenyezi Mungu aliteremsha vitabu vya hekima katika usiku huu uliobarikiwa: “Naapa kwa Kitabu kinachobainisha.  Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji."

Kama vile Qur'ani ilivyojaa kheri inayoenea kwa wale wanaoirejea, usiku wa Qadr vile vile umejaa wema. Yeyote anayeuthamini usiku huu na kujitahidi kuuishi atapata baraka tele. Qur'ani Tukufu inautaja usiku huu kuwa bora kuliko miezi elfu moja: " Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu" (Surah Qadr, aya ya 3).

Usiku huu pia ni muhimu kwani ni usiku ambao Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW). Wafasiri wanaamini kwamba Qur'ani iliteremshwa mara moja usiku huu. Kufuatia haya, Qur'ani Tukufu iliteremshwa hatua kwa hatua kwa muda wa miaka 23.

Usiku wa Hatima pia ni usiku wa amri, ambapo hatima ya watu binafsi na mambo ya kidunia huamuliwa. Katika usiku huu, "malaika na Roho" hushuka duniani ili kudhihirisha hatima ya ulimwengu kwa mwaka ujao: " Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo." (Surah Qadr, aya ya 4).

Kama ilivyoelezwa katika Aya ya nne ya Surah Ad-Dukhan, mambo yote yamefafanuliwa na kubainishwa kwa mujibu wa hekima ya Mwenyezi Mungu katika usiku huu: “Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima.”

Mwisho, usiku huu pia unajulikana kwa msamaha wa dhambi. Imepokewa kuwa katika mwezi wa Ramadhani mashetani hufungwa minyororo na milango ya mbinguni hufunguliwa milango kwa waumini. Mtume Muhammad (SAW) amenukuliwa akisema: “Mwenye kuhuisha usiku wa Qadr ni Muumini na akaiamini Siku ya Kiyama, atasamehewa madhambi yake yote.

3487760

captcha