IQNA

Kongamano la 30 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu laanza Tehran

13:02 - December 15, 2016
Habari ID: 3470744
IQNA-Kongamano la 30 la Kimataifa la Umoja kati ya Kiislamu limeanza asubuhi ya leo mjini Tehran huku maudhui kuu ikiwa ni udharura wa kupambana na makundi ya kitakfiri.

Kongamano hilo la kila mwaka limefunguliwa rasmi kwa hotuba ya Rais Hassan Rouhani na kuhudhuriwa na maulama, wasomi na wanafikra wa Kiislamu zaidi ya 300 kutoka nchi mbalimbali za dunia.

Mkutano huo wa kimataifa ambao utaendelea kwa siku tatu utakuwa na vikao 10 vya kitaalamu ikiwa ni pamoja na kamisheni zinazojadili suala la kupambana na changamoto zinazoukabili Umma wa Kiislamu, hali ya wafuasi wa dini za wachache, umoja wa maulamaa wa muqawama, vyombo vya habari, na kamisheni inayohusiana na masuala ya wanawake.

Sambamba na Mkutano huo wa Umoja wa Kiislamu, kunafanyika tamasha la kwanza la kimataifa la filamu na umoja wa Kiislamu likishirikisha filamu kutoka nchi 37 zinazohusiana na masuala ya ulimwengu wa Kiislamu, shakhsia ya Mtume Muhammad (saw), Qur'ani tukufu, umoja kati ya Waislamu, na vita na propaganda chafu zinazofanywa dhidi ya Uislamu.  

Habari kamili kuhusu ufunguzi wa mkutano huo na hotuba ya Rais Hassan Rouhani itakujieni katika matangazo yetu yajayo. 

Kwa kauli ya Ahul Sunna, Mtume Muhammad SAW alizaliwa tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal huku Wanachuoni wa madhehebu ya Shia wakiamini alizaliwa tarehe 17 Rabiul Awwal. Kwa msingi huo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya Umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa Ulimwengu wa Kiislamu.

3554217

captcha