IQNA

Wiki ya Umoja wa Kiislamu

Umoja wa Kiislamu ni muhimu kwa Kukabiliana na Changamoto zinazowakabili Vijana

20:44 - September 30, 2023
Habari ID: 3477673
TEHRAN (IQNA) – Profesa wa chuo kikuu kutoka Syria amesema kizazi cha vijana katika ulimwengu wa Kiislamu kinakabiliwa na mtanziko wa kiutamaduni na ili kukabiliana na suala hili, kuimarisha ushirikiano na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu ni muhimu.

Dakta Anwar Warda katika hotuba yake katika warsha ya mtandaoni au webinar ya Kongamano la 37 la Umoja wa Kiislamu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano mbele ya masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kielimu.

Ameonya kuhusu hali iliyopo katika ulimwengu wa Kiislamu kuwa ni hali ya kutetereka kutokana na maendeleo ya teknolojia na kusema ni vigumu kubainisha madhara yako wapi kwani mapinduzi ya teknolojia yamewezesha uhamishaji wa haraka zaidi wa mabilioni ya jumbe na data kila siku.

Alisema kutokana na maendeleo hayo ya teknolojia, kizazi cha sasa kinakabiliwa na matatizo mbalimbali.

Alipongeza Mkutano wa 37 wa Umoja wa Kiislamu kwa mada yake ya "Ushirikiano wa Kiislamu ili kufikia Maadili ya Pamoja."

Aliongeza, "Majadiliano hayo yatafungua macho ya kizazi kijacho na kuwawezesha kujua hatua sahihi na kutambua njia sahihi."

Kongamano la 37 la Umoja wa Kiislamu linaendelea katika mji mkuu Tehran huku idadi kubwa ya wanazuoni wa Kishia na Kisuni wakihudhuria kikao hicho kwa njia ya mtandao au intaneti

Mwaka huu wasomi na watu wa dini wanaohudhuria hafla hiyo wanajadili mada "Ushirikiano wa Kiislamu ili kufikia Maadili ya Pamoja". Mkutano wa ana kwa ana katika ukumbi utaanza kesho Okotaba mosi.

Mkutano wa kimataifa ulianza Septemba 28 na utaendelea hadi Oktoba 3 sambamba na Wiki ya Umoja wa Kiislamu ambayo inaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (PBUH).

3485377

Habari zinazohusiana
captcha