IQNA – Mwenyekiti wa Kamati ya Qur’ani ya Jumuiya ya Ulinganiaji wa Kiislamu nchini Libya ametangaza kuchapishwa upya kwa Qur’ani ya taifa (Mus’haf wa Taifa wa Libya) kwa ajili ya kusambazwa bure kwa wananchi.
IQNA – Kwa maamuzi kwamba Hijabu inapunguza taswira ya kutokuwa na upendeleo wa mahakama, jopo la majaji nchini Ujerumani limezuia mwanamke Mwislamu kuhudumu kama jaji.
IQNA – Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) mjini Tehran litakuwa mwenyeji wa moja ya matukio makubwa ya kielimu na kiutamaduni ya mwaka huu mwishoni mwa mwezi huu.
IQNA – Hatua ya mwisho ya mashindano ya 32 ya Qur’ani Tukufu nchini Misri itafanyika katika ardhi hiyo ya Kiarabu kwa ushiriki wa washindani 158 kutoka nchi 72.
IQNA – Moja ya kumbukumbu za kipekee katika ulimwengu wa Qur’ani ni usomaji wa kihistoria wa qari mashuhuri wa Misri, marehemu Ustadh Abdul Basit Abdul Samad, katika Haram ya Imam Musa Kadhim (AS) mjini Kadhimiya, Baghdad, mwaka 1956.
IQNA – Baraza Kuu la Waislamu Ufaransa (CFCM) limesema waumini wameshtushwa na kuumizwa sana baada ya mtu kuvamia msikiti ulioko kusini-kati mwa Ufaransa na kurarua nakala za Qur’ani Tukufu kisha kuzitupa chini.
IQNA – Papa Leo XIV amehudhuria mkutano wa dini mbalimbali uliofanyika katika Uwanja wa Mashahidi jijini Beirut, ambapo walikusanyika mapatriaki wa Kikristo wa Lebanon pamoja na viongozi wa Kiroho wa Kiislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia na halikadhalika dini ya Druze chini ya hema moja.
IQNA – Umoja wa Makari na Wahifadhi wa Qur’ani Tukufu nchini Misri umetangaza kuundwa kwa kamati maalum itakayoshughulikia ufuatiliaji wa utendaji wa makari na kushughulikia malalamiko yanayohusu usomaji wao.