IQNA-Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imesisitiza kuwa, kuainishwa hatima na kufanya maamuzi kuhusu mustakbali wa Syria ni jukumu la pekee la wananchi wa nchi hiyo bila ya uingiliaji uharibifu wala kulazimishwa na mataifa ya kigeni.
IQNA - Mashindano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri yameanza jana kwa usomaji wa aya za Qur'ani na Sheikh Ahmed Nuaina katika Masjid Misr katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala wa Misri.
IQNA - Harakati ya upinzani ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza mahala alipozikwa Sayed Hashem Safieddine, mkuu wa Halmashauri Kuu ya harakati hiyo ambaye aliuawa shahidi mwezi Oktoba.
IQNA-Serikali ya Syria ilianguka mapema Jumapili katika mwisho wa kushangaza kwa uongozi wa miaka 24 wa Rais Bashar al-Assad katika nchi hiyo ya Kiarabu baada ya kundi la wanamgambo wa Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) kuvamia na kuuteka mji mkuu Damascus.
IQNA - Kitengo cha wanawake katika fainali za Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran kiliendeleza shughuli zake katika mji wa Tabriz, mkoa wa Azerbaijan Mashariki tarehe 4 Desemba 2024.
IQNA – Hujjatul Islam Mohseni Qomi, Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alisifu misimamo ya Mufti Mkuu wa Russia kuhusu masuala ya kimataifa na kikanda.
IQNA - Utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kwa nguvu zote kusambaratisha mhimili wa muqawama Asia Magharibi na kutenganisha makundi ya muqawama huko Iraq, Syria na Lebanon, amesema mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Iraq.
IQNA – Mamlaka ya Jumla ya Saudi Arabia kwa Utunzaji wa Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume imetoa seti ya miongozo tisa kwa mahujaji wa kike, lengo likiwa ni kuhakikisha mazingira yenye mpangilio na heshima kwenye maeneo hayo matakatifu.
IQNA-Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano mapya ya kila wiki katika mji mkuu Sana'a na miji kadhaa nchini humo kusisitiza uungaji mkono wao kwa Wapalestina wanaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel.
IQNA - Kulingana na data ya hivi punde kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa Uingereza (ONS), Muhammad limekuwa jina la mtoto maarufu zaidi la wavulana England na Wales mnamo 2023.
IQNA-Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uamuzi wake wa kuanzisha Akademia ya Qur'ani jijini Dar al-Nur na kuahidi kutoa ushirikiano unaohitajika katika uwanja huo.