Tarjuma hizo zimechapishwa katika Taasisi ya Mfalme Fahd ya Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu na zimeonyeshwa kwenye banda la Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia.
Taasisi hiyo iko katika mji mtakatifu wa Madina na huchapisha takriban nakala milioni 10 za Qur'ani kila mwaka.
Pia huchapisha tarjuma za Qur'ani Tukufu katika lugha mbalimbali. Katika maonyesho hayo pia kuna aplikesheni za Kiislamu, filamu za hali halisi, huduma za maktaba ya kielektroniki na vipeperushi kuhusu huduma za Hijja na Umrah.
Taasisi ya Mfalme Fahd ya Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu imetangaza kuwa itasambaza Misahafu 110,000 za katika maonyesho hayo.
Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Sharjah ynafanyika kwa muda wa siku 11 kuanzia Novemba 2 hadi 13 huko Sharjah, Umoja Falme za Kiarabu.
"Eneza Neno" ndiyo kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu.
4097190