Kuomba kibali cha kufanya Umrah wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani sasa kunapatikana kupitia program au apu ya Nusuk ya Saudi Arabia, Wizara ya Hajj na Umrah ilisema mapema wiki hii.
Wizara hiyo ilitoa wito kwa waumini wa Kiislamu kutekeleza Umrah mara moja tu wakati wa Ramadhani ili kuruhusu waumini wengi zaidi kushiriki katika ibada hiyo.
Nusuk, ambayo hapo awali iliitwa Eatmarna, ni jukwaa rasmi la Ufalme wa Saudia la kupanga Hija na Umrah na kupanga safari nzima kuanzia maombi ya eVisa hadi kupanga nafasi ya malazi na safari ya ndege.
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatarajiwa kuangukia Machi 22 au 23 kwa kutegemea mwezi mwandamo.
3482756