IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Dua za Kila Siku za Mwezi wa Ramadhani- Siku ya 22

Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Ramadan Daily Supplications: Day 22

Ee Mwenyezi Mungu! Nifungulie katika mwezi huu milango ya fadhila zako, na Uniteremshie katika mwezi huu baraka zako Uniwafikie katika mwezi huu niyatende yanifikishayo kwenye Radhi yako, Uniweke katika pepo yako uipendayo ewe Mwitika wa maombi ya wenye dhiki.

Kishikizo: dua za kila siku ، ramadhani