IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran yamalizika kwa mafanikio

12:03 - April 03, 2024
Habari ID: 3478626
IQNA - Maonyesho 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalifikia tamati Jumanne usiku.

Maonyesho hayo ya kila mwaka yalifunguliwa mnamo Machi 20 katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini na yalimalizika kwa mafanikio ambapo idadi ya waliotembelea mwaka huu imeongezeka.

Maonyesho hayo yaliwasilisha programu nyingi za Qur'ani, mashindano, na burudani zinazolenga vijana. Sehemu shirikishi, zenye shughuli nyingi kama vile mashindano ya kuhifadhi Qur'ani, michezo ya video, maonyesho ya filamu, matukio ya uhalisia ni kati ya mambo yaliyovutia vijana.

Juhudi kama vile "Hafiz Sho" (kuwa hafidh wa Qur'ani) zilianzishwa na kupongezwa na waliohudhuria. Wakati huohuo, idara, iliyosimamiwa na wataalamu wa Hauza (seminari za Kiislamu), ilitoa majibu kwa maswali ya kidini.

Sehemu ya kimataifa ilishirikisha wawakilishi kutoka nchi 25, wakionyesha michango yao ya Qur'ani.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini Iran na katika uga wa kimataifa.

Huonyesha mafanikio ya hivi karibuni zaidi ya Qur'ani nchini  na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

3487786

captcha