Katika video hii, Ali Dqaa anasoma aya kutoka katika Kitabu Kitakatifu na kisha anawaombea ushindi watu wa Ukanda wa Gaza.
Anasoma Aya ya 5 ya Sura ya Israa:
“ Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa."
Utawala wa Israel ulianzisha mashambulizi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023.
Zaidi ya Wapalestina 34,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa huko Gaza, na wengine zaidi ya 76,800 wamejeruhiwa katika kampeni hiyo ya ukatili wa utawala dhalimu wa Israel.
4211402