IQNA – Kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu mjini Tehran imetoa mwito kwa umma kushiriki katika kuchagua kauli mbiu ya toleo la 33 la tukio hili kubwa la Qur’an.
IQNA – Kiwanda cha Mfalme Fahd cha Kuchapisha Qur’an kilichoko mjini Madina, Saudi Arabia, kilipokea wageni wapatao milioni moja kutoka ndani na nje ya nchi mwaka uliopita.
IQNA – Katika hatua ya kutambua historia na mchango wa Waislamu wake, Jimbo la New York limetangaza mwezi wa Januari kuwa Mwezi wa Urithi wa Waislamu wa Marekani.
IQNA –Ibada ya Itikafu (kujitenga kwa ajili ya ibada msikitini) katika mwezi wa Rajab kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria imefanyika kuanzia Jumamosi asubuhi hadi Jumatatu jioni katika misikiti na maeneo matukufu kote Iran.
IQNA – Ili kuunga mkono ndoa na familia, mjasiriamali mmoja kutoka Jordan ametangaza kuwa vijana watakaohifadhi juzuu sita za Qur’ani Tukufu watapewa msaada wa kifedha pindi watakapooana.
IQNA – Televisheni ya Thaqalayn Satellite imetangaza mpango wa kuandaa mashindano ya tatu ya kimataifa ya Qur’ani yanayojulikana kama “Wa Rattil” katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.
IQNA – Kipindi cha 12 cha mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Dawlat al-Tilawa nchini Misri kiligeuka safari ya kiroho na kihisia, ambapo simulizi binafsi ziliungana na sauti za mbinguni, zikazalisha athari ya kina iliyogusa nyoyo za kila msikilizaji.
IQNA – Mjadala maalum kuhusu “Wajibu wa Umma wa Kiislamu katika kukabiliana na udhalilishaji wa Qur’ani na matukufu mengine na maadui” umefanyika mjini Sanaa, mji mkuu wa Yemen.
IQNA – Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, qari mashuhuri wa Misri, amechapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook video inayoonyesha mwanamke Mmarekani akisilimu katika moja ya misikiti nchini Marekani.
IQNA – Reza Safdari, qari mashuhuri kutoka mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini mashariki mwa Iran, amejiunga na kundi la wanaofuzu kuingia fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika nchini Qatar.
IQNA – Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon imesisitiza katika taarifa yake kwamba watu wa Venezuela, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, watazima njama ya Marekani. Wameongeza kuwa mataifa huru na yenye mamlaka yao yanapaswa kusimama pamoja kukabiliana na dhulma na jinai za Marekani na kuunda ushirikiano wa kimkakati.
IQNA – Sheikh Chems-Eddine Hafiz, mlezi wa Msikiti Mkuu wa Paris, amesema mwaka 2025 ulikuwa miongoni mwa miaka migumu zaidi kwa Waislamu nchini Ufaransa, ukitawaliwa na matukio ya vurugu yaliyofikia kiwango cha “kuuawa kwa misingi ya dini.”